Home  |  Search  |  Help  |  Contact Us  |  Rutgers University Swahili


Practice
101 Assignments
101 Exercises
102 Assignments
102 Exercises
201 Exercises
202 Exercises
Discussion
Your Name:
Your Student ID:
Your E-Mail Address:
The professor's E-mail Address:


Somo la ishirini na nne

SIKU YA KARAMU

 

Suleiman aliamka asubuhi, akaenda kumwamshaHassan.

Akamwuliza, "Ni siku gani leo?’

Hassan akamwambia, "Leo ni Jumamosi. Baba yetu atamchinja kondoo wetumnono leo. Sijui atamchinja saa ngapi. Nitakwenda kumtazama kondoo wetu."

Suleiman na Hassan wakafika kibandani,wakafungua mlango, lakini hawakumwona kondoo.

Suleiman akauliza, "Ni nani amemtoa kondookibandani? Labda yuko nyuma ya kibandani."

Wakatoka nje, wakazunguka kibanda, wakamwonakondoo huko.

Hassan akasema, ‘Labda ni baba yetu. Angalia, ameleta maji kwa sufuria."

Mara wakamwona mama yao amechukua majani ya migomba. Akatandika chinivizuri; kisha akawaambia Suleiman na Hassan walete majani mengine kutokashambani. Suleiman na Hassan wakaenda shambani, wakaona mzigo mwingine wamajani. Suleiman akauchukua.

Hassan akasema, "Sioni mzigo mwingine. Basi nitarudi bila mzigo.

Akamfuata Suleiman. Mama yake Hassan akamwona, akasema, "Hassan, hunakazi. Basi, nenda jikoni ulete visu viwili. Viko juu ya meza ndogo. Halafumwambie baba yako aje; tuko tayari."

Hassan akaenda jikoni, akachukua visu viwili; halafu akamwambia babayake aende kuchinja kondoo.

Baba yake Hassan akaangalia visu, akasema, "Visu hivi haviwezi kuchinjakondoo. Nenda ulete kisu changu."

Hassan akauliza, Kisu chako kiko wapi ?"

Baba yake Hassan akasema, "Kiko katika sanduku langu."

Hassan akaenda, akaleta kisu cha baba yake. Baba yake akachukua kisu,akaenda kumchinja kondoo. Akafunga miguu; kisha akamwangusha chini, akamwambiaSuleiman na Hassan wamsaidie kushika kondoo.

Mama watoto akasema, "Hebu niende. Sitaki kuona."

Baba yake Suleiman akamchinja kondoo; halafu akaanza kumchuna. Watotowalifurahi kuona jinsi ya kuchuna kondoo.

Baba yao alimlaza kondoo kwa mgongo, akakata ngozi kutoka shingoni mpaka katikati ya miguu ya nyuma; halafu akakata ngozi miguuni kwa ndani; halafu akatumia kidole gumba kumchuna kondoo. Alichuna kwa haraka sana. Mama watoto alipomwita,alikataa kwenda; akasema ngozi itaharibika.

Suleiman akamwuliza, "Sielewi. Kwa nini ngozi itaharibika?"

Baba yake Suleiman akamwambia, "Ni rahisi kumchuna kondoo sasa kwa sababu mwili wake una moto."

Alipokwisha kuchuna ngozi, alimweka kondoo juu ya majani ya mgomba. Halafu akaanza kumpasua kifuani, akatoa sehemu za matumbo, akampa Suleiman, akamwambia, "Ondoa mavi matumboni; kisha usafishe matumbo kwa maji."

Baba watoto akaendelea kukatakata nyama ya kondoo katika vipande vingi. Akamwambia Hassan atie vipande hivyo katika sufuria kubwa.

Suleiman akaleta matumbo, akasema, "Nimeosha matumbo. Nafikiri ni safi."

Baba yake Suleiman akaangalia; kisha akasema, "Peleka jikoni; kisha uweke katika chombo chenye maji safi, lakini usiweke kciribu na vitu vyenye uchafu. Kisha uniletee sufuria ndogo pamoja na maji."

Suleiman akapeleka matumbo jikoni. Akaleta sufuria ndogo.

Baba yake Suleiman akatazama sufuria, akasema,"Umeleta sufuria bila maji. Si neno."

Akatafuta nyama nyororo, akakatakata vipande vidogo sana; kisha akachukua vipande hivyo jikoni. Akatia nyama hizo katika matumbo makubwa; halafu akashona. Mama watoto akachukua matumbo hayo pamoja na nyama nyingine, akatia ndani ya sufuria yenye maji. Wakatia sufuria hiyomekoni.

Baba watotoakawaita watoto nje, akasema, "Chukueni vifagio na vikapu. Wenye vifagio wafagie na wenye vikapu waokote takataka kila mahali kwa sababu wageni watafika alasiri."

Watoto wakafagia na wakaokota takataka kila mahali.

Baba watoto akatengeneza moto nje; kishaakaanza kuchoma nyama. Mama watoto akapika ugali kwa sababu wageni hawatapendakula nyama bila chakula kidogo.

Wakati wa saa nane wageni wakaanza kufikakaramuni. Baba watoto akawasalimu wageni; wakaanza karamu. Watoto wakamsaidiamama yao kuwapa wageni vyakula.


Kufahamu


1. Suleiman aliamka asubuhi, akafanya nini?



2. Ni nani alimtoa kondoo kibandani?



3. Kwa nini Hassan alirudi bila kuchukuamzigo?



4. Kwa nini baba watoto alikataa visu?



5. Kwa nini baba watoto alimchuna kondoo kwa haraka?



6. Kwa nini ilikuwa rahisi kumchuna kondoo wakati huo?



7. Suleiman alifanya nini na matumbo?



8. Baba yake Suleiman alimwambia Suleiman amletee nini pamoja na maji?



9. Ni nani walifagia nje?



10. Wageni hawatapenda kula nini?




Sarufi

A. Tunga maneno ya kila kundi yawe sentensi. 

Kwa mfano: mlinzi, wevi, kuona, mlangoni, huyo, jana yatungwe kuwa

--> Jana, mlinzi huyo aliwaona wevi mlangoni.


1. kesho, tatu, eropleni,kuruka, kutoka, mpaka, Nairobi, Dar-es-Salaam




2. mwaka, katika, 1963, wa,kupata, Kenya, uhuru, wake




3. juzi, huyo, kupanda,mkulima, mbegu, shambani




4. sasa, hivi, kuandika,mwalimu, ubaoni, chaki, kwa




5. shingo, ni, twiga, la, refu,shingo, kuliko, la, ng’ombe




B. Geuza sentensi zifuatazo zionyeshe kuwa kitendo kimempata mtu anayetajwa katika alama kama hizi: 

Kwa mfano: Tajiri yule alimpa rafiki yake pesa nyingi. (mimi) igeuzwe kuwa:

--> Tajiri yule alinipa pesa nyingi.


1. Mtoto alimletea baba yake gazeti. (wewe)




2. Msafiri alimwambia rafiki yake habari za nchi mbalimbali. (mimi)




3. Mwalimu atiwapa wanafunzi vitabu vya Kiswahili. (sisi)




4. Wafanyi kazi walimsaidia mtu kujenga nyumba kubwa. (ninyi)




5. Daktari mkuu alimpa mgonjwa dawa nzuri. (wewe)




6. Gari lilimharibikia Dillon njiani. (Amyna Angelique)




 

Once you hit SUBMIT, the results will be e-mailed to your professor with a timestamp



Reference
362
Grammar
Vocabulary

Special Characters
Instructors Notes


© 2002 Rutgers University, excluding excerpted material that remains under the ownership of the existing copyright holders.

digiclass_help@brokenmail.rutgers.edu please replace "brokenmail" with ctaar.rutgers.edu