IM1.jpg)
Mtoto hapo juu
anaogeshwa na mama yake. Wote wawili, mama na mtoto wake, ni wakaaji wa Afrika
Kusini.
Mtoto alikuwa nje akichezacheza na
watoto wengine na sasa ni mchafu kidogo. Lakini kwa kuwa ni mtoto mdogo, hawezi
kuoga peke yake. Kwa hiyo, anahitaji mtu wa kumwogesha. Hii ni kazi ama ya mama
yake au ndugu zake ambao ni wakubwa kuliko yeye.
Picha hii hapo juu ilipigwa zamani
wakati Waafrika wa Afrika Kusini hawakuwa na uhuru halisi kwenye nchi yao.
Walikandamizwa, kuonewa, na kunyimwa haki zao za kiraia na Makaburu walowezi wa
nchi hiyo.
Leo (mwaka
wa 2002) mambo mengi yamebadilika nchini Afrika Kusini. Jambo moja muhimu ni
kwamba serikali ni ya walio wengi. Yaani Waafrika wana sauti nchini kwao.
Kwa sababu hiyo, Waafrika wana uhuru wa kweli. Lakini kwa bahati mbaya, Waafrika
wengi bado ni maskini, wengine maskini
hohehahe.