Wahusika
Mtoa
muhtasari
mtu anayetoa muhtasari wa mtiririko wa vitendo pamoja na maelezo ya
wahusika ndio nani na nani; habari hizi zatolewa kwa Kiingereza [Bi Maswali]
Mzee Mkali
mume mzee wa Mama Furaha; hataki mchezo [Mwalimu]
Mama Furaha
mke kijana wa Mzee Mkali; apenda kutembea nje na vijana wa kiume wa rika
lake [Bi Mjuaji]
Furaha
binti wa Mzee Mkali na Mama Furaha
[Bi Betty]
Sitaki
kijana mpole [Bw Shil]
Wabeya wawili wanawake wa kawaida
wanaokaakaa mitaani [Bi Nancy na Bi Megan]
Saada
mchumbake Sitaki [Bi
Carol]
Msomaji wa barua mtu asomaye barua ya
kimapenzi ya Mama Furaha [Bi Jane]
Mfasiri wa
barua mtu
anayefasiri kwa Kiingereza ile barua ya kimapenzi ya Mama Furaha [Bi
Maswali]
-------------------------------------------------------------------
Mtoa muthasari:
Hamjambo nyote. On behalf of the students of Kiswahili at
Rutgers
University, I would like to extend a
hearty welcome to each and everyone of you. I thank you for coming and I feel
quite confident that you will enjoy our short play entitled “Msiba wa
Kujitakia.” The word “msiba” in Kiswahili means a misfortune, a calamity, a
tragedy, or some infelicitious circumstance. The title, “Msiba wa Kujitakia,”
hence means a self-induced tragedy. The title is in reality an abbreviation of a
Kiswahili proverb that says “Msiba wa kujitakia hauna kilio” which means roughly
that one shouldn’t expect sympathy and understanding for trouble that he or she
has caused by his or her own actions.
This play, which was written jointly by the students in second and third
year Kiswahili, has seven characters. They are:
Mzee Mkali, an elderly man with a very young wife;
Mama Furaha, the young and very flirtatious wife of
Mzee Mkali;
Furaha, the teenage and quite urbanized daughter of
Mzee Mkali and Mama Furaha;
Sitaki, a young man who is polite and somewhat
shy;
Saada, the fiancée of Sitaki;
Two busybody women, who spend a large part of each day
gossiping among themselves.
The first scene opens in the home of Mzee Mkali with him telling his wife
that he’s going to town and that he might be late in returning. He also informs
her that a young acquaintance named Sitaki will be dropping by and that she
should tell him not to wait, that they will meet another day.
Onyesha la
Kwanza
Onyesho hili linaanza na
Mama Furaha, mkewe Mzee Mkali, anashughulika na usafi nyumbani kwao. Baada ya
kupita nukta 15 hadi 20 hivi, anaingia Mzee
Mkali.
Mzee
Mkali:
Mama Furaha!
Mama
Furaha:
Abee.
Mzee
Mkali:
Mimi natoka kidogo, naenda mjini. Nina shughuli moja muhimu. Siwezi kujua
kwa hakika lakini huenda ikawa nitachelewa kurudi.
Mama
Furaha:
Haya mume wangu. Nenda salama urudi salama.
Mzee
Mkali:
Haya, nitajaribu kuharakisha mambo lakini unajua mambo yalivyo mjini siku
hizi na ahadi za uwongo.
Oh, nilitaka kusahau --- atakuja yule kijana Sitaki kuonana nami.
Mwambie samahani, nitaonana naye siku nyingine.
Mama
Furaha:
[akitabasamu na kuonyesha kufurahi
sana] Sawa mume
wangu.
Mzee Mkali anageuka na
kuondoka.
[PAZIA]
Mtoa
muthasari: Scene
two opens with Mama Furaha making herself attractive in hopes of attracting the
attention of the young man who will be stopping by to see Mzee Mkali, who as we
know, has gone to town. Mama Furaha’s young and impulsive teenage daughter tells
her that she is going to the movie with a young male friend and this upsets Mama
Furaha. The daughter makes a fast exit when the young man, Sitaki, arrives. The
rest of scene is devoted to Mama Furaha and her attempts at seducing
Sitaki.
Onyesho la
Pili
Mzee akitoka Mama Furaha
anaanza kujipambapamba. Ghafla binti yake anatokea. Anamwambia mamake
anatoka.
Furaha:
Mama, mama, mimi naenda sinema.
Mama Furaha:
Nini? Unaenda wapi? Sinema? Sasa hivi? Unaenda na
nani?
Furaha:
Na rafiki yangu.
Mama Furaha:
Rafiki yako nani? Si yule mhuni Hamisi?
Furaha:
Mamaaa, yeye si ….
Wakati huohuo sauti
inasikika mlangoni ikibisha hodi. Furaha anaenda mlangoni na kuufungua.
Furaha:
Ohh, karibu, karibu Bw Sitaki.
Akiingia Bw Sitaki, wakati
uleule Furaha anatoka nje huku anakimbia. Anasikika kusema, “Kwa heri
mama!”
Mama Furaha:
[akisema kwa sauti
nyororo] Karibu Ndugu Sitaki,
karibu, karibu sana.
Sitaki:
Asante Mama Furaha. Habari za hapa
nyumbani?
Mama Furaha:
Salama kabisa. Mambo hapa nyumbani poa. Tuko wazima wote. Habari za
utokako wewe?
Sitaki:
Sisi twamshukuru Mwenyezi, sote ni wazima wa afya.
Mama
Furaha:
Na mimi nimefurahi kusikia hayo.
[Nukta 5 hivi zinapita katika hali
ya ukimya.]
Mama Furaha:
Karibu ukae kaka.
Sitaki:
[uso wake ukionyesha
wasiwasi] Mzee
yupo?
Mama Furaha:
Hayupo, katoka kidogo, ameenda mjini. Lakini amesema atarudi moja kwa
moja.
Sitaki:
[akionyesha kusitasita kidogo]
Ahh, labda niende.
Mama Furaha:
Kaa bwana mdogo, usiende. Haki ya Mungu hatachelewa kurudi. Ataingia sasa
hivi.
[Anamwonyesha kiti na kumwashiria
akae. Sitaki, akionyesha wasiwasi, anakalia kiti polepole na
taratibu.]
Nikuletee nini? Kuna soda,
kuna maji, kuna maji ya matunda, kuna chai, na kahawa.
Sitaki:
[akionyesha kufikiri kidogo.]
Nadhani chai itanitosha.
Mama
Furaha:
Haya nakuja.
[Anageuka na kuondoka. Akiwa
jikoni, kabla hajaanza kushughulika na utayarishaji wa chai ya mgeni, anaonekana
akiandika harakaharaka maneno fulani kwenye karatasi. Kumaliza hayo,
anakunjakunja karatasi hiyo na kuitia mfukoni mwake.
Baada ya dakika moja hivi kupita
Mama Furaha anarudi huku akibeba sinia yenye kikombe, birika, kijiko, na sukari.
Anaweka sinia juu ya kimeza na kukivuta kimeza hicho mbele ya
Sitaki.]
Karibu chai. Leo hakuna
maziwa kwa hiyo ni chai ya rangi tu. Samahani.
Sitaki:
Bila samahani. Chai ya rangi inatosha kabisa. Ahsante Mama
Furaha.
Mama Furaha:
[akikaa kwenye kiti karibu na
kijana Sitaki.] Ni muda mrefu hatujakuona. Mbona unatususa hivi?
Sitaki:
Siwasusi ila nilikuwa na kazi nyingi.
[Nukta mbili tatu za kimya
zinapita. Sitaki anakunywa chai yake huku Mama Furaha anamkodolea macho … macho
ya huba. Wasiwasi wa Sitaki wazidi
kuongezeka. Mwishowe inambidi Sitaki
kuuliza.]
Mama Furaha, una hakika Mzee atarudi sasa hivi? Hatachelewa
mjini?
Mama Furaha:
[Anamjibu huku anamkodolea macho
ya “wasiwasi ondoa kijana mwenzangu, mimi ni wako” …] Amesema hatachelewa.
Lakini hata akichelewa kidogo, naona si vibaya, siyo?
[Anasogeza kiti chake karibu naye
na anaanza kumpapasapapasa mabegani huku akitamka hivi:] Kwa kweli, mimi natumai atachelewa
sana tupate kujuana vizuri zaidi
au siyo kijana mwenzangu?
Sitaki:
[akionyesha kuogopa] Mimi
nadhani bora niende sasa. Nitarudi baadaye akisharudi Mzee.
[Anaanza kuinuka toka kwenye kiti
lakini Mama Furaha anamzuia huku anazidi kumpapasapasa na kumwambia maneno ya
huba.]
Mama Furaha:
Usiende mpenzi, nakupenda sana
sana
sana. Usiende mpenzi. Tafadhali
nakuomba. Na ukienda, tuende wote.
[PAZIA]
Mtoa
muthasari: Scene
three opens with two local female gossips outside the house of Mzee Mkali. They
are talking, laughing, slapping five, and pointing towards the house. Suddenly
Bi Saada, the fiancée of Sitaki appears. The two gossips tell her their
suspicions. Saada seems at first not to believe them, but eventually she becomes
pissed off.
Onyesho la
Tatu
Wabeya wawili nje ya nyumba
ya Mzee Mkali wakipigana soga. Wanachekacheka na kugongana viganja. Mmojawao
anaelekeza kidole kwenye nyumba:
Mbeya wa 1:
Ahh, jamani, wanafanya nini humo ndani muda wote huu?
Mbeya wa 2:
Na Mzee hayupo! Lakini si unajua tabia zake Mama Furaha? Basi, ole wao
Mzee akiwafumania leo. Huyo mzee ni moto wa kuotea mbali, ni mtu wa hatari
kwelikweli. Hana mchezo.
Saada
[Wakati huohuo anatokea Bi Saada, mchumbake Sitaki] Vipi shoga,
unaongea juu ya nani? Kulikoni nyumbani kwa Mzee Mkali?
[Wote wanaangua vicheko]. .
Mbeya wa 1:
Bi Saada, nafikiri mali yako iko hatarini dada
yangu. Yule mwizi wa mitaani Mama Furaha anajaribu kupindua kitanda chako.
Mchumbako Sitaki yumo ndani, yuko naye, na Mzee Mkali hayupo. Wako peke
yao.
Saada kwanza anaonyesha kutoamini lakini baadaye sura yake yabadilika
na kuonyesha kaudhika sana.
[PAZIA]
Mtoa
muhtasari: This
is the fourth and final scene. This is where Mama Furaha is caught red handed
and her infidelity exposed. Happily, however, Sitaki and his fiancée, Bi Saada,
are still in love and their relationship remains intact. Check it out.