Home  |  Search  |  Help  |  Contact Us  |  Rutgers University Swahili


Practice
101 Assignments
101 Exercises
102 Assignments
102 Exercises
201 Exercises
202 Exercises
Discussion
 

HABARI ZA KOMBO NA ZAINABU

 

 

Huyu ni Kombo. Kombo ni mvulana. Alizaliwa Dar es Salaam lakini sasa anaishi Marekani. Yeye ni mwanafunzi wa shule ya msingi. Yeye ni mwanafunzi mzuri na anapenda masomo yake.

 

Maswali

1.   Mtoto huyu anaitwa nani?

2.    Anatoka wapi?

3.    Kombo anaishi wapi sasa?

4.    Je, yeye ni mwanafunzi mbaya?

5.    Kombo anapenda au hapendi masomo yake?

------------------------------------------------------------

 

 

           Huyu ni Zainabu. Yeye ni msichana mdogo. Zainabu anatoka Kenya lakini sasa anaishi Tanzania. Yeye ni mwanafunzi wa shule ya msingi. Anapenda masomo yake na anapenda kucheza na kucheka na rafiki zake.            

 

Maswali

1.    Msichana huyu jina lake ni nani?

2.    Alizaliwa wapi?

3.    Anaishi wapi sasa?

4.    Je, Zainabu ni msichana mkubwa?

5.    Zainabu anapenda masomo yake?

6.    Zainabu anapenda kufanya nini zaidi?    



Reference
362
Grammar
Vocabulary

Special Characters
Instructors Notes


© 2002 Rutgers University, excluding excerpted material that remains under the ownership of the existing copyright holders.

digiclass_help@brokenmail.rutgers.edu please replace "brokenmail" with ctaar.rutgers.edu