Bwana Kofia

Bwana
huyu pichani jina lake ni “Kofia.” Huitwa hivyo kwa sababu siku zote kofia yake
haimtoki kichwani. Yaani yeye kila siku huvaa kofia. Hakuna siku utamkuta
hajavaa kofia yake. Ukimwona Jumatatu, utamwona amevaa kofia yake. Ukimwona
Jumanne, utamwona amevaa kofia yake. Ukimwona Jumatano, pia utamwona amevaa
kofia yake. Ni hali kadhalika kwa siku zote za wiki.
Bwana
Kofia ni mfagizi katika ofisi za Baraza
la Kiswahili la Taifa jijini Dar es Salaam. Yeye ni mfanyakazi mzuri na kazi
zake huzifanya kwa bidii. Ni Mwislamu na ana mke na watoto.